Millionaire  Ads

Yanga bingwa kwa mara 3 mfululizo, Toto,Lyon zashuka daraja, uchwawi watawala CCM Kirumba, video ya uchawi pia imo




Pazia La Ligi kuu limefungwa rasmi leo huku Yanga wakitangazwa kuwa mabingwa wa Ligi kuu
Jumla ya mechi nane zilipigwa viwanja tofauti nchini na mechi zote zilianza mda mmoja
Simba wakicheza katika Uwanja wa Taifa waliibuka na ushindi wa bao 2-1 magoli ya Simba yakifungwa na Shiza Kichuya kwa penati na Ibrahim Ajib.
Wakati Yanga walikubali kipigo cha goli 1 kwa bila toka Mbao Fc, vitendo vya kichawi vilitawala katika mchezo huu, wachezaji wa Yanga walivamia goli la Mbao wakitafuta uchawi lakini hawakufanikiwa.
bofya hapa kuona video

Yanga wanatwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara 27 baada ya kuwa na uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa kwani timu ya simba ina pointi 68 sawa na Yanga
Huku tukishudia Jkt Ruvu, African Lyon, na Toto African zikishuka daraja.
Matokeo mengine ya Lig kuu.
Mbao FC 1-0 Young Africans
Simba SC 2-1 Mwadui FC
Azam FC  0-1 Kagera Sugar
Mtibwa Sugar 3-1 Toto Africans
Majimaji FC 2-1 Mbeya City
Stand United 2-1 Ruvu Shooting

Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+
0 Comment untuk "Yanga bingwa kwa mara 3 mfululizo, Toto,Lyon zashuka daraja, uchwawi watawala CCM Kirumba, video ya uchawi pia imo"

Back To Top