Timu ya Manchester United ya nchini
England jioni ya leo imewasili mjini Stockholm na kikosi cha wachezaji 20
tayari kwa mchezo wa kesho saa 21:45 usiku.
Wachezaji waliokwenda na timu ni Romero,
De Gea, Pereira, Valencia, Tuanzebe, Fosu-Mensah, Jones, Mitchell, Smalling, Juan
Mata,Darmian, Blind, Herrera, Carrick, Mkhitaryan, McTominay, Harrop, Martial,
Rashford na Rooney.
wachezaji wengine ni majeruhi na beki tegemeo kwa sasa wa United Bailly ana adhabu baada ya kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Celta vigo.
Hii ni zaidi ya fainali kwa united
kwani wanataka kurudi ligi ya mabingwa na njia pekee ni kutwaa kombe hilo ili
kupata nafasi ya moja kwa moja, ikumbukwe ligi kuu ya England hutoa timu tatu
za kwanza kushiriki ligi ya mabingwa mpja kwa moja na timu inayoshika nafasi ya
nne hushindania kushiriki ligi ya mabingwa na timu za nchi nyingine ‘Champion
league play Off’. Man united imeambulia nafasi ya 6 kwenye Msimamo wa ligi
nchini England.
Endapo Man itakosa kombe hilo
itawalazimu kushiriki ligi ya Europa msimu ujao.
Angalia timu ambazo zimelitwaa kombe
hili tangu mwaka 1971/72
1971–72 Tottenham Hotspur
1972–73 Liverpool
1973–74 Feyenoord
1974–75 Borussia Mönchengladbach
1975–76 Liverpool
1976–77 Juventus
1977–78 PSV Eindhoven
1978–79 Borussia Mönchengladbach
1979–80 Eintracht Frankfurt
1980–81 Ipswich Town
1981–82 IFK Göteborg
1982–83 Anderlecht
1983–84 Tottenham Hotspur
1984–85 Real Madrid
1985–86 Real Madrid
1986–87 IFK Göteborg
1987–88 Bayer Leverkusen
1988–89 Napoli
1989–90 Juventus
1990–91 Internazionale
1991–92 Ajax
1992–93 Juventus
1993–94 Internazionale
1994–95 Parma
1995–96 Bayern Munich
1996–97 Schalke 04
1997–98 Internazionale
1998–99 Parma
1999–2000 Galatasaray
2000–01 Liverpool
2001–02 Feyenoord
2002–03 Porto
2003–04 Valencia
2004–05 CSKA Moscow
2005–06 Sevilla
2006–07 Sevilla
2007–08 Zenit Saint Petersburg
2008–09 Shakhtar Donetsk
2009–10 Atlético Madrid
2010–11 Porto
2011–12 Atlético Madrid
2012–13 Chelsea
2013–14 Sevilla
2014–15 Sevilla
2015–16 Sevilla
2016/17 ?
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Man United yawasili Stockholm nchini Swedeni tayari kwa fainali ya Europa ligi dhidi ya Ajax, rekodi tangu 1971/72"