Winga machachari wa timu ya Azam
aliyeko Tenerife kwa mkopo Farid Mussa amezidi kujisafishia njia ya kucheza
kikosi cha kwanza ambacho kinasaka nafasi ya kucheza Laliga msimu ujao.
Farid ambae anatumika kama winga wa
kulia wa timu ya vijana ya Tenerife ameaminiwa na kocha wake Quico de Diego Kutokana
na Uwezo wake mkubwa anaouonyesha uwanjani.
Tangu ajiunge na timu hiyo December
mwaka jana Farid amecheza mechi 13 akiwa na timu ya vijana na
kufunga magoli 6 na kutoa pasi za magoli ‘Assists’ 6.
Timu ya vijana ya Tenerife ilikuwa
inashiriki ligi ya vijana ya ‘Tercera Division’ kanda ya Visiwa vya Canary
iemaliza katika nafasi ya tano.
0 Comment untuk "Nyota ya Farid Mussa yazidi kung'aa, anasubiri hatma ya kocha kumpandisha timu ya wakubwa"