Kamati ya ligi kuu Tanzania maarufu
kama kamati ya saa 72 imetoa maamuzi mazito kwa kilabu ya Yanga Kutokana na
matukio mbalimbali yaliyojitokeza wakati timu hiyo ilipokuwa inacheza baadhi
michezo ya ligi kuu Tanzania Bara, rungu lenyewe lipo hivi:
1.
Wachezaji
Deus Kaseke, Obrey Chirwa na Simon Msuva
wamesimamishwa kucheza ligi kuu kwa mujibu wa kanuni namba 9(5) wakisubiri
hukumu yao baada ya kumzonga mwamuzi Ludovic Charles na kumuangusha katika
mchezo kati ya Mbao na Yanga uliofanyika Ccm Kirumba jijini Mwanza may 20,
2017.
2.
Mchezo
wa may 13, 2017 Yanga vs Mbeya City, Yanga hawakuingia uwanjani kupitia mlango
sahihi hivyo kutozwa faini ya sh laki tano(500000) kwa mujibu wa kanuni namba 14(48).
3.
Siku
hiyohiyo ya may 13 baada ya mchezo kumalizika Washabiki wa Yanga walivunja uzio
wakiingia uwanjani kusherekea ubingwa, na hivyo kamati imeamuru Yanga kulipa
hasara hiyo iliyotokea kwa mujibu wa kanuni namba 42(3) ya Ligi Kuu
4.
Kamati
imeitoza Yanga shilingi milioni moja (1000000) kwa mujibu wa kanuni namba 14(48)
ya Ligi Kuu ya kwa kosa la kugoma kuingia vyumbani katika mchezo wa may 9, 2017
dhidi ya Toto Africans.
5.
Kamati
pia imeitoza Yanga shilingi laki tano (500000) Kutokana na Imani za
kishirikina, Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 42(1) ya Ligi
Kuu.
Millionaire Ads
0 Comment untuk " Rungu kali la kamati ya ligi latua Jangwani walimwa faini kibao, Msuva na wenzake nje ligi kuu "