Fainal ya ASFC kuchezeshwa na
mwamuzi toka Dodoma
Kwa mujibu wa Afisa habari na
mawasiliano wa bwana Alfred Lucas TFF imemteua Ahmed Kikumbo
kupuliza filimbi katika mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho Tanzania kati
ya Simba SC na Mbao FC siku ya jumamosi may 27,2017 katika dimba la Jamhuri
mjini Dodoma.
Waamuzi wasaidizi ni Mohammed
Mkono kutoka Tanga na Omari Juma kutoka Dodoma, mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon kutoka
Dodoma, kamishina wa mchezo atakuwa ni Peter Temu kutoka Arusha.
Tff imeziomba timu zinazocheza
mchezo huo, waamuzi na Washabiki kufanya mchezo uwe wa amani na kuzitakia kilalakheri
pande zote zinazohusika na mchezo huo
Mchezo huo utakuwa saa kumi kamili
jioni.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Simba SC vs Mbao FC, Fainal ya ASFC kuchezeshwa na mwamuzi toka Dodoma"