Msimu huu Jose Mourinho amecheza kwa
mipango huku akisema yeye ni kocha wa mataji kwa kutwaa makombe mawili, kombe
la kwanza lilikuwa ni kombe la ligi maarufu kama Carling Cup, na badae jana
usiku kutwaa kombe la ligi ya Europa.
Pongezi ziende kwa Poul Pogba na
Henrikh Mkhitaryan kwa magoli yao katika dakika 18 na 48 ambayo ndio
yameipeleka United kuwaka rekodi ya aina yake Duniani.
United kwa England ndio timu pekee
iliyochukua makombe yote ya vilabu, ligi ya mabingwa ulaya, Europa ligi na
kombe la vilabu Duniani.
Manchester united inaungana na Ajax,
Chelsea, Juventus and Bayern Munich kuwa timu zilizotwaa mataji yote ya ulaya.
Jose Mourinho alistahili kutwaa
kombe hili kwa kuwa aliweka mkazo zaidi kuhakikisha analichukua na kupuuzia
ligi kuu ya England.
Sasa tunaweza kusema kuwa Manchester
United wamepitia mlango wa uani Kuelekea ligi ya mabingwa.
0 Comment untuk "Timu ya Manchester united imetwaa kombe la Europa ligi baada ya kuichapa Ajax 2 – 0, na kupata tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa 2017/2018."