Tanzania
jana imekwenda sare na timu ya Angola na kuendelea kuongoza kundi lake la A
baada ya kujikusanyia pointi 4 na magoli 2 huku mpinzani wake mkubwa wa kundi
hilo akiwa ni Angola ambayo ina pointi 4 na goli 1.
Endapo Tanzania
itafanikiwa kutwaa usukani wa kundi A basi itatinga Robo fainali na kukutana na
wenyeji Afrika Kusini ambao wao wamepangwa kuanzia hatua hiyo ya Robofainali.
Kiungo mchezeshaji
wa Tanzania Mzamiru Yassin ndie aliekuwa mwiba mchungu kwa Angola kwani
alikamata dimba vilivyo na kufanya atakalo huku akipiga pasi za uhakika kwa
washambuliaji wa Tanzania ambao jana walikamatwa ipasavyo.
Tanzania iliwakilishwa
na Manula, Kapombe, Gadiel, Banda, Mbonde,
Nyoni,Mao,Maguri,Msuva,kichuya,Mzamiru
0 Comment untuk "Angola 0 - 0 Tanzania, Picha kibao mechi ya Jana,Tanzania yaongoza kundi A, kutinga Robo Fainali endapo itaifunga Mauritius"