Liverpool
wamemuulizia winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, ambaye huenda
akagharimu pauni milioni 25, huku Manchester City na Chelsea pia wakimnyatia
(Mirror).
Manchester
City wana uhakika wa kumsajili beki kutoka Brazil anayechezea Juventus Dani
Alves wiki hii. Chelsea na Tottenham pia wanamtaka Alves (Sun).
Manchester
City wana matumaini ya kukamilisha usajili wa mabeki watatu kabla ya kwenda
Marekani mwezi ujao kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya. Miongoni
mwao wanatarajia kufanikisha uhamisho wa Dani Alves na Kyle Walker (Daily
Mail).
Mshambuliaji
wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, amekutana na meneja wa Manchester City
Pep Guardiola, kuzungumzia uwezekano wa kuhamia Etihad (Le 10 Foot).
Atletico
Madrid wanafikiria kumchukua Olivier Giroud (Tuttosport).
Meneja wa
Chelsea Antonio Conte anafikiria kumchukua winga wa Sevilla, Vitolo, 27, kwa
pauni milioni 35 (Daily Mirror).
Manchester
United wana uhakika wa kumsajili kiungo wa Chelsea Nemanja Matic, 28, wiki hii
kwa takriban pauni milioni 40. Hata hivyo Jose Mourinho alikuwa akimtaka zaidi
Eric Dier au Radja Nainggolan kabla ya Matic (Telegraph).
Inter Milan
wamewaambia Manchester United watoe pauni milioni 44 kama wanamtaka Ivan
Perisic
(Gazzetta
dello Sport).
Mshambuliaji
Naby Keita anayesakwa na Liverpool hatoruhusiwa kuondoka Leipzig bila malipo
yasiyopungua pauni milioni 70 (Guardian).
Leicester
City watalazimika kulipa takriban pauni milioni 40 iwapo wanataka kumsajili
kiungo mshambuliaji wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27 (Leicester Mercury).
West ham
wanajiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kulipa zaidi ya pauni milioni 20
kumchukua mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30 (Telegraph).
West Ham
wapo tayari kulipa pauni milioni 50 kuwachukua Theo Walcott na Olivier Giroud
kutoka Arsenal (Daily Star).
West Ham pia
wanamtaka mshambuliaji wa Sampdoria, Luis Muriel, 26 (Sun).
AC Milan
wamemfanya beki wa kati wa Arsenal Laurent Koscielny, kuwa kipaumbele cha
usajili, wakati klabu hiyo ya Seria A ikitaka kuimarisha safu yake ya ulinzi
(Telefoot).
Lyon
wameacha kumfuatilia Olivier Giroud, huku rais wa klabu hiyo akidai kuwa
Arsenal hawataki kumuuza (Evening Standard).
Tottenham
wameambiwa watahitajika kulipa pauni milioni 26 ili kumsajili kiungo Adrien
Silva, 28, kutoka Sporting Lisbon ya Ureno (Record).
Kiungo
mshambuliaji wa Leicester City Riyad Mahrez, 26, anafikiria kusaini mkataba wa
miaka minne ambao amepewa na Arsenal, baada ya kuchoka kuwasubiri Barcelona
(Sport).
Kiungo
mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez, 25, anayesakwa na Manchester
United huenda akabakia Spain, ikiwa Cristiano Ronaldo, 32, ataondoka (Don
Balon).
Trabzonspor
ya Uturuki inazungumza na Liverpool kuhusu usajili wa Lucas Leiva, 30
(Fotomac).
Barcelona
wanazungumza na kiungo wa zamani wa Tottenham, Paulinho, 28, anayechezea
Guangzhou Evergrande (Sky Sports).
Barcelona
watamtaka tu Paulinho iwapo watashindwa kumsajiliRiyad Mahrez, 24, kutoka
PSG (Daily Mail).
Beki wa
Manchester City Aleksander Kolarov, 31, amesema siku moja anataka kurejea
katika klabu yake ya zamani, Lazio (Il Messaggero).
Bayern
Munich wanataka kumsajili kiungo wa Schalke Leon Goretzka, 22, mwisho wa msimu
ujao ambapo atakuwa mchezaji huru (Kicker).
C&P from S. Kikeke
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA SIKU YA JUMANNE 27.06.2017"