Arsenal wamejitoa katika mbio za
kumwania nyota wa Monaco Kylian Mbappe, 18, na sasa wataelekeza nguvu zao
kumpata Alexandre Lacazette na Thomas Lemar (Mail Online).
Mesut Ozil ameonesha dalili za
kubakia Arsenal baada ya kulipia tena chumba maalum cha kutazamia mpira
(executive box) ndani ya uwanja wa Emirates (The Sun).
Antonio Conte hajafurahishwa na
hatua ya Chelsea kumfuatilia Romelu Lukaku badala ya Andrea Belotti. Conte
ameghadhibishwa kwa sababu wachezaji hao wawili bei yao ni moja, takriban pauni
milioni 85, lakini mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea Michael Emenalo ameamua
kumfuatilia Lukaku badala ya Belotti (Daily Star).
Guangzhou Evergrande hawana mpango
wowote wa kumuuza Paulinho kwenda Barcelona (Nanfang Daily).
Liverpool wapo tayari kupanda dau la
pauni milioni 70 kumtaka kiungo wa kimataifa wa Guinea Naby Keita, 22
anayeichezea RB Leipzig (Mirror).
Liverpool wanataka kuwasajili Naby
Keita pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain, 23 (Liverpool Echo).
Liverpool wanataka kumsajili beki wa
kushoto Andrew Robertson kutoka Hull City (Liverpool Echo).
Real Madrid huenda wakamsajili Eden
Hazard, 26, kutoka Chelsea na Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco (Diario
Madrista).
Everton watakamilisha usajili wa
mshambuliaji wa Malaga, Sandro, 21, wiki ijayo (Liverpool Echo).
Alvaro Morata amewaambia marafiki
wake kuwa ameamua kujiunga na Manchester United na kuwa mkataba tayari
“umekamilika” (Daily Express).
Manchester United hawatomuuza Ander
Herera kwenda Barcelona, licha ya taarifa kusema Barca watafikiria kumchukua
iwapo watamkosa Marco Verratti, 24, kutoka PSG (Independent).
Barcelona wanamtaka Ander Herera na
Riyad Mahrez, kama watashindwa kumsajili Marco Verratti (Sport.es).
Radja Nainggolan anayesakwa na
Manchester United, huenda akajiunga na Inter Milan, baada ya klabu hiyo ya
Italia kutoa dau la euro milioni 60 (101 Great Goals).
Jose Mourinho anafikiria kumchukua
kiungo wa Middlesbrough Marten de Roon katika wiki chache zijazo (TuttoMercatoWeb).
Manchester City wameanza mazungumzo
na Tottenham kuhusiana na beki wa kulia Kyle Walker, lakini Spurs hawataki
kupokea chochote chini ya pauni milioni 50 (The Mirror).
Manchester City huenda wakaamua
kumfuatilia winga wa Bayern Munich Kinglesy Coman (RMC).
Chelsea wanafikiria kumfuatilia beki
wa Roma, Kostas Minolas, 26, ambaye alikuwa anakaribia kujiunga na Zenith St
Petersburg kwa pauni milioni 26 (London Evening Standard).
Meneja wa Chelsea Antonio Conte
anaghadhibishwa na jinsi klabu yake inavyoendesha shughuli za usajili (Star).
Real Madrid bado wanamtaka
mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, licha ya klabu hiyo kusema haina mpango wa
kumuuza mchezaji huyo kutoka Ubelgiji (OK Diario).
Chelsea wanajiandaa kutaka kupanda
dau kwa beki wa Bayern Munich Jerome Boateng (Daily Mirror).
Chelsea wanakabiliwa na ushindani
kutoka kwa PSG katika kumsajili beki wa Juventus Alex Sandro (The Mirror).
Southampton wanamtaka mshambuliaji
wa Manchester City Kelechi Iheanacho, 20 ambaye thamani yake ni pauni milioni
25 (Sun).
Meneja wa Watfrod Marco Silva
amedhamiria kumsajili Kieran Gibbs, 27, kutoka Arsenal. Beki huyo pia
amehusishwa na kuhamia Liverpool (Mirror).
Monaco hawatarajii kumuuza Thomas
Lemar, 21, msimu huu, na wamewaambia Arsenal na Tottenham kuwa mchezaji huyo
hauzwi (Independent).
Licha ya tamko hilo, Barcelona nao
wamesema wanamtaka Thomas Lemar (L’Equipe).
Mshamnuliaji wa zamani wa Arsenal na
Manchester United Robin van Persie huenda akarejea katika EPL msimu ujao na
kujiunga na Crystal Palace (Daily Mirror).
Meneja mpya wa Nantes, Claudio
Ranieri anamtaka kipa wa Arsenal David Ospina (France Football).
Meneja wa Brighton Chris Hughton
amethibitisha kuwa klabu yake imewasiliana na Liverpool kuhusu kumsajili beki
Joe Gomes, 20 (Brighton Argus).
Beki wa Hull City Andy Robertson,
23, anasakwa na Liverpool, kwa sababu Jurgen Klopp anataka kusajili beki mpya
wa kushoto (Liverpool Echo).
Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness
amesema hawatomsajili Alexis Sanchez, 28, kutoka Arsenal, kwa kuwa klabu yake
inazingatia kusajili wachezaji chipukizi (Kicker).
Mtoto wa Zinedine Zidane, Enzo, 22,
ameondoka Real Madrid na kujiunga na Alves kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu,
baada ya kukosa namba katika timu inayofundishwa na baba yake (FourFourTwo)
Kiungo Saul Niguez, 22, anataka
kubakia Atletico Madrid, lakini huku Barcelona na Manchester United zikimtaka,
anasema angependa kupata pesa zaidi (Goal).
Mwenyekiti wa West ham David Gold
amesema hawamfuatilii Jack Wilshere, 25, lakini klabu yake inatafuta
washambuliaji wawili wapya na wenye uzoefu wa EPL (TalkSport).
Newcastle wanakaribia kumsajili beki
wa Eibar, Florian Lejeune, 26, na pia wanataka kumshawishi Andre Gray, 26
kutoka Burnley (Newcastle Chronicle).
Na hatimaye…..
Mshambuliaji wa Real Madrid,
Cristiano Ronaldo ameonesha picha ya mapacha wake na kusema “Nina furaha sana
ya kuweza kuwabeba wapenzi wangu wapya katika maisha yangu”.
Habari zilizothibitishwa tutakujuza
mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi
usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Nb: C&P from Salim Kikeke
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 30.06.2017"