Kocha mkuu wa taifa stars Salum
Mayanga amefanya mabadiliko machache katika kikosi chake Kuelekea mchezo wa
Stars dhidi ya Rwanda kuwania kucheza mashindano ya kombe la Afrika kwa
wachezaji wa ndani maarufu kama CHAN.
Amewatema wachezaji wote wanaocheza
ligi nje ya Tanzania na kuwajumuisha wengine kutoka ligi ya Tanzania katika
kikosi hicho
Wachezaji walioachwa ni Pamoja na
Thomas Ulimwengu, na
Katika kikosi hicho Mayanga amefanya
mabadiliko kidogo upande wa kipa kwa kumuita kipa wa Serengeti Boys Ramadhani
Kambwil na kumuacha kipa wa mabingwa wa soka Tanzania bara Beno Kakolanya.
Kikosi kinakachoenda kukipiga na
Rwanda Tarehe 15 July 10, 2017 Mwanza kipo hivi:
Makipa: Aish Manula, Said Mohammed
na Ramadhani Kabwili.
Mabeki: Shomari Kapombe, Hassan
Kessy, Gardiel Michael, Hamimu Abdul, Boniface Maganga, Salim Mbonde, Abdi
Banda na Nurdin Chona.
Viungo: Muzamil Yassin, Himid Mao, Raphael
Daud, Erasto Nyoni, Said Ndemla, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Joseph na Mahundi Salmin Hoza.
Washambuliaji: John Bocco, Kelvin
Sabato, Athanas Mdamu na Stahmil
Mbonde.
0 Comment untuk "Kakolanya wa Yanga OUT Kambwili wa Serengeti Boys IN Stars vs Rwanda Mwanza"