Kamati ya nidhamu ya
shirikisho la soka nchini Tanzania TFF chini ya mwenyekiti wake Tarimba Abbas
imeamuachia huru Manara na baadhi ya wadau wengine wa soka waliokuwa kifungoni
kwa vipindi tofauti.
Sababu za kuachiwa huru
kwao ni Kutokana na baadhi yao akiwemo manara kuiandikia kamati hiyo kuipitia
upya hukumu yao na kuomba wapunguziwe adhabu hizo walizopewa.
Kamati imewaacha rasmi
huru wafuatao:
1. Haji
Manara msemaji wa timu ya Simba SC
2. Ayubu
Myaulingo ambeye ni mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Rukwa.
3. Blassy
kiondo ambaye ni kaimu katibu mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa
4. James
Makwinya Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Rukwa
Tarimba amesema "Wale
ambao hawakuwasilisha kutaka kupitiwa upya kwa hukumu zao, tumewaambia TFF nao
walifanyie kazi hilo. Kama watataka kuona inafanyika review basi haki
itendeke"
Baada
ya kupata msamaha huo Manara aliahidi yafuatayo:
“Nawaahidi
kuendelea kufanya kazi zangu kwa weledi, nidhamu na kwa kuzingatia miiko ya
mchezo huu, unaobeba dhamana za maisha ya watu walio wengi, sambamba na
kuendelea kuitetea na kuilinda klabu yangu kwa nguvu zote,”.
Hayo
ni maneno ya Manara
0 Comment untuk "Kamati yamtoa Manara kifungoni"