Ripoti toka kwa madaktari wanaomtibu
mshambuliaji wa timu ya Yanga Donald Dombo Ngoma wamemruhusu mchezaji huyo
kuanza mazoezi baada ya vipimo vya mwisho kuonyesha kuwa yupo ‘FIT’.
Ngoma atajiunga na wenzake ndani ya
wiki hii baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini alipokwenda kufanyiwa vipimo
kilisema Chanzo cha habari hiyo.
Ngoma ambae alikuwa gumzo baada ya
kuhusishwa kujiunga na Simba lakini alirejea na kusaini mkataba wa miaka miwili
na Yanga.
Ujio wa Ngoma ni furaha tosha kwa
mashabiki na benchi la ufundi ambapo sasa litakuwa na wigo wa kuamua nani aanze
kikosi cha kwanza baina ya wachezaji Ngoma, Chirwa, Tambwe na Ajib.
Wakati huohuo kipa namba moja ndani
ya Yanga Deo Munish ameanza mazoezi na timu ya Yanga kwa ajili ya maandalizi ya
ngao ya jamii, msimu mpya wa ligi, kombe la shirikisho la Azam na kilab bingwa
Afrika.
0 Comment untuk "RIPOTI YA MADAKTARI: NGOMA RUKSA KUICHEZEA YANGA MSIMU HUU, DIDA NAE AANZA MAZOEZI NA YANGA"