Beki wa Southampton Virgil van Dijk,
26, huenda bado akahamia Liverpool kwa pauni milioni 60 msimu huu. Mchezaji
huyo amesisitiza anataka tu kwenda Liverpool. (Sun)
Arsenal wanafikiria kutoa pauni
milioni 45 kumtaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Express)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa
amepigwa picha kwenye Instagram akiwa amevaa jezi ya Atletico Marid na kuandika
“mpe salaam zangu Conte”. (Mail)
Chelsea wanataka kumsajili
mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya
kumkosa Romelu Lukaku, 24. (Sky)
Chelsea wameonywa na Borussia
Dortmund kuwa wana wiki moja tu ya kumsajili Pierre Emerick-Aubameyang. (The
Sun)
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger
anadhani kuwa ataweza kumshawishi Alexis Sanchez, kutoondoka Emirates. (Mirror)
Vinginevyo Arsene Wenger anafikikia
kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Celtic, Moussa Dembele, 20. (Star)
Arsene Wenger amekata tama ya
kumsajili Kylian Mbappe, 18, na badala yake sasa anaelekeza nguvu katika
kumsajili Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco. (Telegraph)
Arsenal pia wanafikiria kumsajili
mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, kuziba nafasi ya Alexis Sanchez
ikiwa ataondoka. (Don Balon)
Thomas Lemar ameitaka klabu yake ya
Monaco kumuuza kwenda Arsenal. (sun)
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny
anakaribia kuhamia Juventus kwa pauni milioni 8. (Daily Mirror)
Chelsea wanataka kumsajili
mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29. (Star)
Chelsea wapo tayari kumpa mkataba wa
miaka mitano winga wa Atletico Madrid Yannick Carasco, 23. (Don Balon)
Meneja wa Manchester United Jose
Mourinho anataka Toni Kroos, 27, kuwa sehemu ya mkataba wowote utakaomhusisha
David de Gea kwenda Real Madrid. (Sun)
Manchester United wanaonekana
kukaribia kumpata kiungo wa Inter Milan Ivan Perisic. (Daily Mirror)
Zlatan Ibrahimovic amekataa nafasi
ya kujiunga na LA Galaxy na anapanga kusaini mkataba mpya na Manchester United.
(The Sun)
Paris Saint-Germain wanapanga kutoa
euro milioni 150 kumtaka mshambuliaji wa Real Madrid Marco Asensio. (Don Balon)
AC Milan wananamnyatia mshambuliaji
wa Real Madrid Alvaro Morata, 24. (Gazzetta dello Sport)
Barcelona wapo tayari kutoa euro
milioni 65 pamoja na Ivan Rakitic ili kumsajili Marco Verratti kutoka PSG.
Calciomercato)
Tottenham wanataka kujaribu tena
kumsajili kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. Timu hizo mbili zimeshindwa
kukubaliana ada ya uhamisho ya mchezaji huyo. (Independent)
Tottenham wana matumaini ya
kukamilisha usajili wa beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19, mwishoni mwa wiki
hii. (Mirror)
Loic Remy, 30, anatazamiwa kuondoka
Chelsea msimu huu, huku Everton na Southampton zikimtaka. (Metro)
West Ham watapanda dau la tatu
kumtaka winga wa Stoke Marco Arnautovic, 28, baada ya dau la awali kukataliwa.
(Sky Sports)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza
mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi
usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
source: salim kikeke
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMATATU JULY 17,2017"