Msemaji wa timu ya Ndanda ya mtwara wana kuchele
Indrisa Bandari ameiambia jamii fm Radio ya mkoani mtwara kuwa timu yao kesho
jumatatu inaanza rasmi mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu Tanzania Bara."tutafanya
mazoezi mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni," alisema Bandari
Kuhusu suala la timu kutokuwa na kocha Bandari
alisema kuanzia sasa muda wowote watamtangaza kocha wao, wapo kwenye mazungumzo
ya kukamilisha mkataba.
Alipoulizwa kuhusu fukuzafukuza ya makocha ndani ya
timu hiyo bandari alisema "ndanda haifukuzi mwalimu tunaangalia ‘commitments’
ya mkataba ipoje, tunaangalia mkataba wake upoje akishindwa kufikia matarajio
ya mkataba, mwalimu anaondoka".
Kuhusu suala la usajili Bandari aliwataja baadhi ya
wachezaji ambao mpaka sasa wameshasajiliwa na timu hiyo kuwa ni Ibrahim Job,
Jabir Azizi, na kuahidi kuwa wapo vijana wengine watano ambao anategemea
kuwatangaza kesho.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "NDANDA KUANZA MAZOEZI RASMI KESHO TAYARI KWA MSIMU UJAO"