Mfungaji
bora wa muda wote wa timu ya Manchester United Wyne Rooney (31) amejiunga na
timu yake ya zamani baada ya kuondoka mika 13 iliyopita yaani 2004 kwa ada ya
uhamisho ya £27m.
Rooney
amesaini kandarasi ya miaka miwili na washiriki wa Europa Ligi msimu ujao
akitokea Manchester United aliyoichezea michezo 559 na kuifungia jumla ya
magoli 253 yanayomfanya awe ndie mchezaji aliefunga magoli mengi zaidi ndani ya
timu hiyo akimuacha Bobby Charlton mwenye magoli 249 katika michezo 758 ndani
ya Manchester United.
Rooney
katika maisha yake ndani ya United amefanikiwa kutwaa vikombe vyote ngazi ya kilab ikiwemo ligi ya mabingwa mwaka
2008, kilab bingwa Dunia, Europa Ligi, FA, Carling Cup,ligi kuu, ngao ya jamii.
0 Comment untuk "Rooney arudi Everton akiwa mchezaji huru, Asaini mkataba wa miaka miwili"