Paris Saint-Germain wanataka
kuwapiku Manchester City katika dakika za mwisho na kumsajili Dani Alves. Beki
huyo kutoka Brazil alionekana kukaribia kuhamia City lakini PSG huenda
wakamchukua (Le10Sport).
Wakala wa James Rodriguez amewaambia
Liverpool, Manchester United, Inter Milan, Juventus, Manchester City na PSG
kuwa wanaweza kumsajili kiungo huyo wa Real Madrid, lakini hakuna kati ya timu
hizo iko tayari kutoa euro milioni 75 wanazotaka Real, ambao wanataka kumuuza
kutokana na kuwasili kwa Dani Caballos (SPORT).
Beki wa Southampton Virgil van Dijk
ameiambia klabu yake kuwa anataka kuhamia Liverpool tu (Mirror).
Manchester United wapo tayari
kuwapiga kumbo jingine Chelsea kwa kumsajili James Rodriguez. Chelsea na PSG
zinamtaka mchezaji huyo lakini James mwenyewe angependa kwenda kwa Mourinho
(Express).
Baada ya kuwazidi kete Chelsea
katika kumsajili Romelu Lukaku, Manchester United wanataka kuwapiku tena katika
kumsajili kiungo Tiemoue Bakayoko kutoka Monaco, ambao wamekasirishwa na kasi
ndogo ya Chelsea kumfuatilia mchezaji huyo. United watamchukua ikiwa
watashindwa kumpata Nemanja Matic kutoka Chelsea (The Sun).
James Rodrigues anataka kuhakikisha
anaondoka Real Madrid katika saa 48 zijazo ili asisafiri na Real Madrid kwenda
Marekani katika mechi za kabla ya kuanza kwa msimu (AS).
Arsenal wamekubaliana maslahi
binafsi na Thomas Lemar ya mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki, lakini bado
hawajafikia makubaliano na Monaco (the Sun).
Celta Vigo wanafikiria kumchukua
winga wa Borussia Dortmund Emre Mor ambaye pia amehusishwa na Liverpool
(Atlantico).
Dani Ceballos, 20, amekubali mkataba
wa miaka sita kujiunga na Real Madrid kutoka Real Betis na atakamilisha mkataba
wa euro milioni 18. Barcelona walikuwa ‘wakimchombeza’ mchezaji huyo (Marca).
Antonio Rudiger anakaribia
kukamilisha uhamisho wake kutoka Roma kwenda Chelsea kwa pauni milioni 34 na
mkataba utakamilika katika saa 24-48 zijazo (Sky).
Arsenal wameweka wazi kuwa
hawatomuuza Alexis Sanchez au Alex Oxlade- Chamberlain kwenda katika timu
yoyote hasimu ya EPL. Sanchez ananyatiwa na Manchester City huku
Oxlade-Chamberlain akihusishwa na Liverpool (Daily Star).
Arsenal watakuwa tayari kumuuza
Alexis Sanchez kwenda Manchester City ikiwa tu watatoa pauni milioni 80
(Mirror).
Arsenal wameongeza dau lao hadi
pauni milioni 40 kutaka kumsajili winga Thomas Lemar, 21 kutoka Monaco, baada
ya pauni milioni 35 za awali kukataliwa (L’Equipe).
Meneja Antonio Conte atarejea Chelsea
siku ya Jumatatu kutoka likizo na kutaka mazungumzo na klabu hiyo kuhusu
kushindwa kumsajili Romelu Lukaku kutoka Everton (Express).
Nahodha wa Manchester United Wayne
Rooney, 31, amefanya vipimo vya afya Everton (Sky Sports).
Zlatan Ibrahimovic, 35, huenda
akapewa mkataba mpya na Manchester United baada ya kupona jeraha la goti
(Mirror).
Tottenham wamesema kiungo wao Eric
Dier, 23, hauzwi kwa bei yoyote. Hii ni baada ya kuhusishwa na Manchester
United kwa pauni milioni 50 (Mail).
Jose Mourinho ameongeza juhudi za
majadiliano kutaka kumsajili James Rodriguez, 25, kutoka Real Madrid. Real
wanataka pauni milioni 62 (Independent).
Newcastle wamekuwa na mazungumzo na
Middlesbrough ya kutaka kumsajili winga Adama Traore, 21 ambaye huenda
akagharimu hadi pauni milioni 20 (Chronicle).
Newcastle wapo tayari kulipa euro
milioni 20 kumsajili Andreas Samaris kutoka Benfica (O Jogo).
Kiungo wa Bayern Munich Douglas
Costa anakaribia kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwenda Juventus na huenda
akahamia moja kwa moja baadaye kwa euro milioni 40 (La Stampa).
source: Salim Kikeke
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAPILI 09.07.2017"