Mtanzania Mbwana Samatta jana usiku
alifanya kile kinachotabiriwa na wengi huenda akawa mfungaji bora wa Belgium baada
ya jana kuanza vyema.
Genk na Waasland-Beveren walitoka
sare ya 3- 3 lakini kitu kizuri kwa watanzania ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania
kufanya yake.
Waasland-Beveren ndio wa kwanza
kujipatia magoli mawili, dakika ya 45 Oliver Myny alifunga goli la kwanza,
mnamo dakika ya 47, Zinho Gano alipachika goli la pili na kufanya wageni hao
waongoze kwa goli hizo mbili.
Genk walisubiri mpaka dakika ya 70
ndio wakafungua ukurasa wa magoli kupitia kwa Naranjo, 80’ Samatta akachoa na
ubao ukasomeka 2 – 2.
Dakika ya 82 Genk kupitia kwa Leandro
Trossard walipata goli la 3.
Wakiamini kuwa mpira umeisha ghafla
dakika ya 90 Waasland-Beveren kupitia kwa Zinho Gano walisawazisha na mchezo
kuhitimishwa kwa sare ya 3 – 3.
matokeo mengine ni:
Millionaire Ads
matokeo mengine ni:
Lokeren 0 - 4 Club Brugge
Eupen 0 - 5 Zulte-Waregem
Sporting Charleroi 1 - 0 Kortrijk
0 Comment untuk "Samatta aliamsha dude Belgium - First Division A, atupia na kutengeneza moja"