Moja ya mada kuu zitakazojadiliwa ni
uwezekano wa kubadili kalenda ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ili
isiingiliane na ratiba ya ligi za Ulaya. Kombe la Mataifa hufanyika mwezi
Januari wakati ligi za Ulaya zimepamba moto, na wachezaji muhimu hulazimika
kwenda kuchezea timu zao za taifa, pia watajadili kuhusu mashindano yaliyochini
ya CAF ngazi ya vilabu nk.
Mkutano huo utaongozwa na Ahmad
Ahmad ambae ndie rais wa sasa wa CAF aliyechukua mikoba ya Rais aliyedumu kwa
miaka 29 ndani ya Shirikisho hiyo Issa Hayatou.
Wadau mbalimbali wapatao zaidi ya
400 wanategemewa kuhudhuria mkutano huo akiwemo kocha wa mabingwa wa ligi ya MabingwaUlaya
Real Madrid Zinedine Zidane.
Hayo yanafanyika kabla ya mkutano
mkuu wa CAF utakaofanyika july 20 na july 21 na kuwashirikisha washirika wake
wote 56.
0 Comment untuk " Shirikisho la Mpira barani Afrika CAF linafanya mkutano wa siku mbili nchini Morocco"