Mabingwa wa England, Chelsea wana
“nia thabiti” ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 29.
(Sky Sport)
Chelsea wanazungumza na Manchester
City kuhusiana na usajili wa Sergio Aguero. (beIN Sporst)
Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic
hayuko tayari kulipa fedha nyingi kumsajili Alvaro Morata, 24, kutoka Real
Madrid, huku kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo anaelekea Italia. (Star)
Chelsea wanafikiria kumrejesha tena
Stamford Bridge, beki wa Southampton Ryan Bertrand. (Evening Standard)
Chelsea wanataka kukamilisha usajili
wa mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang. (Sky Sports)
Dau la pauni milioni 2.6 la
Manchester City kumtaka kipa wa Napoli, Pepe Reina, 34, limekataliwa. (Mirror)
Manchester City hawatakabiliwa na
ushindani tena kutoka Bayern Munich katika kumsajili Alexis Sanchez, 28, kutoka
Arsenal baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge kusema
hawamfuatilii tena. (Manchester Evening News)
Paris Saint-Germain wameingia katika
mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Alexis sanchez, 28. (Daily
Mirror)
Paris Saint-Germain wapo tayari
“kuvunja benki” kutaka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Neymar, na watakuwa
tayari hata kulipa euro milioni 222, kulazimisha uhamisho wake.
(GianlucaDiMarzio.com)
Washauri wa karibu wa Neymar
wanamshauri aondoke Barcelona ili kuepuka kufunikwa na Lionel Messi. Manchester
City, PSG na Manchester United zote zinamtaka mshambuliaji huyo kutoka Brazil.
(Sport)
Mkurugenzi wa michezo wa Barcelona
amesema hakuna timu itakuwa tayari kutoa pauni milioni 195 kumsajili Neymar,
25. (Mail)
Manchester United wanafikiria
kupanda dau la mwisho la pauni milioni 60 kumtaka kiungo wa Tottenham, Eric
Dier, 23. (Mirror)
Zlatan Ibrahimovic, 35, ameonesha
dalili kuwa atabakia Old Trafford baada na kuwaandikisha watoto wake katika
akademi ya Manchester United. (Sun)
Manchester United wanamtaka kiungo
anayesakwa na Liverpool Naby Keita, 22, huku klabu yake RB Leipzig ikipunguza
vikwazo. Mbali na United na Liverpool, pia Arsenal, Manchester City, Juventus
na Inter Milan zinamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea. (Football
Whispers)
Manchester United wana uhakika wa
kukamilisha usajili wa Ivan Perisic katika saa 48 zijazo. (Starsport)
West Brom wanamtaka beki wa Arsenal
Kieran Gibbs, 27, lakini timu hizo mbili hazijafikia makubaliano yoyote.
(Birmingham Mail)
Arsenal watajaribu kupunguza idadi
kubwa ya wachezaji wake wasiotumika, kabla ya kufanya uamuzi wa kuvunja rekodi
tena ya usajili na kumchukua Thomas Lemar, 21, kutoka Monaco. (Mail)
Monaco wamewaambia Arsenal
watalazimika kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kutoa takriban pauni milioni 80
kumsajili kiungo Thomas Lemar, 21. (The Mirror)
Arsenal wamekataa dau la pauni milioni
6.2 kutoka Sampdoria la kutaka kumsajili kiungo Jack Wilshere, 25. Arsenal
wanataka pauni milioni 8.8. (DI Marzio)
Juventus wanataka kuimarisha kiungo
chao kwa kumsajili Nemanja Matic, 28, au Steven N’Zonzi, au William Carvalho.
(Calciomercato)
Inter Milan wanapanga kuwajaribu
Real Madrid kwa kutoa dau kubwa kumtaka kiungo Toni Kroos. (Sport Mediaset)
Crystal Palace wanakaribia kumsajili
beki wa Ajax, Jairo Riedewald, 20 kwa pauni milioni 8. (Evening Standard)
Crystal Palace wanataka kuimarisha
kiungo chao kwa kumchukua Jack Wilshere kutoka Arsenal kwa mkopo. (The Sun)
Crystal Palace wapo tayari kutoa
pauni milioni 16 kumsajili beki wa Arsenal Callum Chambers, 22. (Telegraph)
Beki wa kushoto wa Nice ya Ufaransa
Dalbert Henrique, 23, amethibitisha kuwa Liverpool wanamtaka, lakini amesema
dau kutoka Inter Milan ni la kuvutia zaidi. (Express)
Riyad Mahrez, 26, yuko tayari
kupunguziwa mshahara ili aweze kujiunga na Roma. (Leicester Mercury)
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny,
27, anakaribia kujiunga na Juventus. (Guardian)
Winga wa Hull City, Ahmed
Elmohamady, 29, anakaribia kujiunga na Aston Villa. (Hull Daily Mail)
Beki wa kushoto wa Hull City Andy
Robertson, 23, anakaribia kujiunga na Liverpool kwa pauni milioni 8. (Liverpool
Echo)
Mshambuliaji wa Manchester City
Wilfried Bony, 28, hajasafiri na kikosi kilichokwenda Marekani na huenda
akarejea tena Swansea. (Wales Online)
Beki Matheiu Debuchy wa Arsenal
anatarajiwa kujiunga na Nice ndani ya saa 48 zijazo, baada ya kushindwa kuwika
Emirates. (Europe1 Sports)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza
mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi
usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
Hayo yanafanyika kabla ya mkutano
mkuu wa CAF utakaofanyika july 20 na july 21 na kuwashirikisha washirika wake
wote 56.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 18.07.2017"