Simba Sports Club
D'salaam, Tanzania
11-7-2017.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
________________
Klabu ya Simba inapenda kutoa
ufafanuzi kuhusiana na malalamiko ya mchezaji Abdi Banda ambae alilalalamika
jana kupitia vyombo vya habari,kuwa klabu imemkatalia kumpa barua ya kumuacha
(REALESE LETTER) ilhali yeye amepata Timu huko Afrika kusini na huku akiwa
amemaliza mkataba wake.
Ni kweli Banda amemaliza Mkataba na
klabu, na jana alikuja ofisini kwetu kutaka barua hiyo, lakini akakumbushwa
kuwa,ukiwa umemaliza Mkataba haupaswi kupewa barua hiyo,wanaoandikiwa barua
hiyo ni waajiriwa ambao bado wana mikataba na labda kwa sababu yoyote ile,klabu
inaamua kuachana nao.
Lakini kwa kuwa Banda aliitaka hyo
barua, akaambiwe aandike barua fupi tu ya kuomba Realese Letter, ili ibaki
kumbukumbu kwa klabu, lakini kwa mshangao wa maafisa wa klabu aligoma
kuiandikia barua klabu na kuamua kukimbilia kwenye vyombo vya habari na Blogs.
Klabu imesikitishwa sana na kitendo
hicho kinachojirudia cha kutafuta huruma kupitia Media,huku akijua kuwa
anaikosea heshima klabu na kuipaka matope bila sababu.
Simba inaamini sana utamaduni wake
wa miaka mingi wa kuwaruhusu wachezaji wake kwenda nje ya nchi kucheza soka,
pindi wapatapo nafasi hiyo,lakini inasisitiza sana suala la utaratibu,haijawahi
kutokea kokote duniani,mchezaji aliyemaliza mkataba kudai Realise letter,na
kiukweli tumeshangazwa pia na baadhi ya vyombo vya habari kulishupalia jambo
hili bila hata kutusikiliza (kubalance story).
Na kwa kupitia barua hii, klabu
inawaambia haitafanya kazi kwa shinikizo la mtu au chombo chochote kile huku
tukifahamu ni kinyume na utaratibu na utamaduni wa mchezo huu unaopendwa
duniani kote.
Mwisho
tunawaambia kwa sasa tutakuwa na
udhibiti mkubwa wa wachezaji wetu na benchi la ufundi kuongea na vyombo vya
habari na blogs, huku pia ikimsisitiza Banda akitaka barua yetu ni wajibu wake
kuandika barua pia,vnginevyo klabu yetu inamtakia mafanikio makubwa huko
aendako.
IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO
SIMBA SC.
SIMBA NGUVU MOJA
Millionaire Ads
0 Comment untuk "SIMBA WATOA UFAFANUZI JUU YA MALALAMIKO ABD BANDA"