Everton wametoa dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27. Wakifanikiwa watakuwa wametuia zaidi ya pauni milioni 100 za usajili msimu huu (Daily Mail).
Baada ya kumsajili Romelu Lukaku,
24, kutoka Everton, Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa Monaco
Tiemoue Bakayoko, 22, baada ya kukubaliana mkataba wa pauni milioni 35. Chelsea
wanamtaka pia Bakayoko (Daily Star).
Arsenal wapo tayari kupanda dau
la tatu la zaidi ya pauni milioni 45 kumtaka winga wa Monaco, Thomas Lemar,
baada ya dau la pauni milioni 30 na 40 kukataliwa (Daily Mirror).
Mshambuliaji wa Arsenal Theo
Walcott, 28, amedhamiria kupigania nafasi yake Emirates, licha ya kuhusishwa na
kuhamia West Ham kwa pauni milioni 20 (Daily Star)
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger
anataka kuimarisha eneo la kiungo kwa kumsajili Marcelo Brozovic kutoka Inter
Milan (ESPN).
Kipa wa Arsenal Wojciech
Szczesny, 27, ambaye amehusishwa na kuhamia Juventus, ameachwa kwenye kikosi
kilichosafiri kwenda Australia kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya
(Sun).
Chelsea wapo tayari kutoa euro
milioni 80 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata baada ya
kumkosa Romelu Lukaku (AS).
Meneja wa Tottenham Mauricio
Pochettino anataka kumsajili beki wa Estudiantes, Juan Foyth, 19 kwa pauni
milioni 10 (Daily Mirror).
Real Madrid wapo tayari kumuuza
kiungo Mateo Kovacic, na Tottenham wamehusishwa na kumchukua mchezaji huyo wa
kimataifa wa Croatia (Evening Standard).
Cristiano Ronaldo atabakia Real
Madrid msimu wa 2017-18 na hivyo kufuta uvumi wa kuhamia Manchester United
(AS).
Newcastle wanajaribu kukamilisha
usajili wa kiungo wa Norwich Jacob Murphy, 22, kwa pauni milioni 8.5, huku
Southampton na Crystal Palace wakimtaka pia mchezaji huyo (Daily Mirror).
Habari zilizothibitishwa tutakujuza
mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi
usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers
0 Comment untuk "TETESI ZA SOKA ULAYA SIKU YA JANA JUMATATU 10.07.2017"