Leo majira ya saa 20:30 usiku timu
ya taifa ya Tanzania Taifa stars itashuka uwanjani kukipiga na timu ya taifa ya
Lesotho katika mchezo wa kuwania mshindi wa tatu katika michuano ya COSAFA.
Mwaka 2015 Lesotho waliifunga Tanzania
goli 1- 0 katika michuano hii ya COSAFA.
Tanzania na Lesotho hii ni mara ya
pili ndani ya mwaka huu wa 2017 kukutana.
Mara ya kwanza kwa mwaka 2017 timu
hizi zilikutana katika michuano ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika katika
Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es salaam na timu hizo kutoka sare ya goli 1 –
1.
Wakati huo Tanzania ilikuwa nafasi
ya 139 katika viwango vya soka duniani wakati Lesotho wao wakikamata nafasi ya
121.
Leo zinakutana ikiwa Tanzania wameipiku
Lesotho kwenye viwango vya ubora vya Dunia, Tanzania ipo nafasi ya 114 Duniani wakati
Lesotho wao wakiwa nafasi 138.
Hii inatoa tafsri kuwa Tanzania ni
lazima washinde mechi leo ili kujiongezea alama katika viwango vya soka Duniani.
Endapo Tanzania itapata Matokeo hasi
basi kuna uwezekano mkubwa tukapoteza alama nyingi kwenye shirikisho la soka
ulimwenguni FIFA.
Hivyo leo kwa Tanzania ni zaidi ya
mechi ya mshindi wa tatu.
0 Comment untuk "TANZANIA VS LESOTHO, COSAFA CUP MSHINDI WA TATU NI ZAIDI YA MECHI KWA TANZANIA"