Timu ya simba SC inaweza kumuuza
mchezaji wake tegemeo kwenye nchi za kiarabu Chanzo kimoja kimeeleza.
Shiza Kichuya huenda nae akafuata nyao
za Saimon Msuva kutimkia nchi za kiarabu baada ya timu moja ambayo haijatajwa
jina lake kuvutiwa na mchezaji huyo.
Timu hiyo ipo tayari kumfanyia
vipimo vya afya pekee na kumjuisha katika kikosi chao bila majaribio endapo
atafuzu vipimo.
Kwa Tanzania ni mwanzo mzuri kwani
baada ya msimu ulioisha wa ligi kuu kumalizika wachezaji maarufu watatu
wamepata timu nje ya nchi tena za ligi kuu.
Wachezaji hao ni Abdi Banda toka
Simba aliyetua Baroka Fc Afrika kusini, Ramadhani Singano ‘Messi’ toka Azam na
Saimon Msuva toka Yanga wawili hawa wapo Difaa Aljadida ya Morocco.
Huu ni mwanzo mzuri kwa soka letu
hasa timu ya taifa.
ikumbukwe pia kiungo wa timu ya Simba Said Ndemla na yeye ametimkia Swedeen kufanya majaribio.
ikumbukwe pia kiungo wa timu ya Simba Said Ndemla na yeye ametimkia Swedeen kufanya majaribio.
Mungu zibariki
Safari za wachezaji wetu Amin.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "YA YANGA KUWAKUTA SIMBA"