SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)
limemzuia kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kucheza mechi ya
Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam Jumatano.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema leo katika mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba, Chirwa hawezi kucheza Jumatano kwa sababu katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC alimsukuma refa mjini Mwanza.
“Chirwa atakukosa mchezo wa Jumatano dhidi ya Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa saa 11:00 mjini Dar es Salaam kutokana na kesi inayomkabili ya kumsukuma mwamuzi aliyechezesha mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC,”alisema.

Chirwa ataendelea kuwa nje hadi
hapo Kamati ya Masaa 72 itakapokutana na kutoa maamuzi dhidi yake.
Wakati huo huo Lucas amewataja marefa watakaochezesha mechi hiyo ni Elly Sasii kutoka Dar es Salaam, atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha na Hellen Mduma.
Viingilio katika mchezo huo ni Sh. 7,000 kwa viti vya rangi ya kijani na bluu, 10,000 Viti vya Orange, 20,000 kwa VIP B ba 25 kwa VIP A .

0 Comment untuk "CHIRWA OUT SIMBA NA YANGA JUMATANO"