Millionaire  Ads

KRC GENK ya Mbwana Samatta yachezea kichapo, Samatta akilamba kadi ya njano


Timu ya Genk ya Ubeligiji jana usiku imepoteza mchezo wake wa ligi kuu nchini humo maarufu kama Belgium - First Division A kwa kutandikikwa goli 2 – 1 na timu ya Standard Liege.
Mchezo huo ambao ulikuwa na jumla ya kadi 7 za njano huku kadi nne zikienda kwa Genk na tatu zikienda kwa Standard Liege.

Genk ndio walikuwa wa kwanza kupata goli mnamo Dakika ya 36, kupitia kwa Siebe Schrijvers baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Bryan Heynen.
Dakika tano badae Samatta alionywa kadi ya njano baada ya kucheza mchezo mchafu.
Standard Liege walijipatia magoli yao kupitia kwa Edmilson Junior 48’ na Paul-Jose M'Poku 63’

Genk wanaendelea wanabaki nafasi ya 11 na pointi 1 baada ya mechi 2, huku Standard Liege wao wakikaa kileleni baada ya kufikisha ponti 4 katika mechi 2.
Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "KRC GENK ya Mbwana Samatta yachezea kichapo, Samatta akilamba kadi ya njano"

Back To Top