Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.
Polisi Morogoro FC imetolewa kundi A na
kupelekwa kundi B.
Mshikamano FC ya Dar es Salaam imetolewa kundi
B na kupelekwa kundi B.
Kundi C halijaguswa.
Makundi kwa sasa yatakuwa hivi:
Kundi A: Ashati United, Friends
Rangers, African Lyon na Mshikamano FC za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya
United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.
Kundi B:
Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es
Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es
Salaam na Polisi Morogoro na Mawezi Market ya Morogoro.
Kundi C:
Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno
Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp
ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
0 Comment untuk "MABADILIKO MAKUNDI YA LIGI DARAJA LA KWANZA"