MBAO
WAPATA MDHAMINI MPYA KULAMBA MILIONI 140 KWA MWAKA.
Ule msemo wa kizuri chajiuza unaendelea kuikuta timu ya Mbao fc
baada ya leo kupata mdhamini mpya wa timu hiyo kutoka kwenye kampuni ya GF
trucks $ Equipment ltd wenye thamani ya shilingi milioni 140.
Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Kulwa Bundala alisema udhamini huo utaendana na kuwapa basi la kusafiria
lenye thamani ya shilingi milioni 70.
"Jumla ya udhamini tulioutoa wa shilingi milioni 140 kati
ya hizo milioni 70 zimetumika kuwanunulia basi la kusafiria na milioni 70
nyingine wamewapa kwa ajili ya matumizi mengine binafsi yatakayoendelesha timu
yao, "alisema Bundala
Basi na jezi za Mbao FC vitakuwa na branded ya GF Trucks &
Equipment, udhamini huo ni wa mwaka mmoja lakini basi ambalo litakuwa branded
na GF Trucks & Equipment litakaa na nembo ya wadhamini kwa miaka miwili.
GF Trucks & Equipment anakuwa mdhamini wa pili baada ya
kampuni ya maziwa ya Cowbel
Millionaire Ads
0 Comment untuk "MBAO WAPATA MDHAMINI MPYA KULAMBA MILIONI 140 KWA MWAKA."