Mchezaji mpya wa Difaa Hassani Jadidi ya nchini
Morocco, mtanzania Simon Msuva ni miongoni mwa wachezaji waliochaguliwa
kutambulisha jezi za timu hiyo kwa msimu ujao.
Na baada ya utambulisho huo timu hiyo ilishuka
uwanjani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya ASO Daraja la Kwanza.
Katika mchezo huo Msuva alifunga goli moja na
kutengeneza goli la ushindi.
Matokeo yalikuwa
2-1 kwa difaa kushinda mchezo huo.
“Tumeshinda mabao 2-1, maana huku kila siku
tunacheza mechi, kweli wenzetu wapo tofauti sana,”amesema Msuva na kuongeza;
“Leo mimi nimefunga la kusawazisha na kutengeneza la ushindi,”.
Millionaire Ads
“Ni mechi ngumu, timu za huku wachezaji wake wapo
fiti sana na wana nguvu na kasi sana, kwa kweli huku wenzetu wapo tofauti
sana,”alisema.
0 Comment untuk "MSUVA ACHAGULIWA KUTAMBULISHA JEZI ZA DIFAA HASSANI JADIDI"