Cristiano, Messi na Neymar
wapitishwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA (The Best FIFA Men's)
Awali majina yalikuwa 24 lakini
yamechujwa na kubakia majina 3.
Wanaofanya kazi hii ni jopo la
makocha wa timu za taifa,makeptein wa timu za taifa, baadhi ya vyombo vya
habari vilivyo chaguliwa na wadau wa soka.
Majina hayo 24 yalianza kuchujwa
tangu August 21 na September 7

Kuna uwezekano mkubwa kwa mchezaji
bora Duniani raia wa Ureno Cristiano Ronaldo kutetea taji lake la FIFA Best
Player of the year.
Uwezekano huo unatokana na mafanikio
aliyoyapata kwa msimu ulioisha ukilinganisha na wapinzani wake Messi na Neymar.
Ronaldo ambae kwa msimu ulipita
aliisaidia timu yake ya taifa kutinga nusu fainali ya kombe la mabara, aliweza
kuisaidia kilabu yake kutwaa ligi ya mabingwa Ulaya, Laliga Pamoja na Uefa Super
Cup, huku Ronaldo akimpiku Messi kwenye ufungaji bora wa ligi ya mabingwa Ulaya.
Kwa upande wa Messi yeye msimu
uliopita alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa laliga na kuambulia kikombe kimoja tu
cha Copa del Rey.
Neymar ambae ndie mchezaji ghali
zaidi Duniani akisajiliwa toka Barcelona kwenda PSG anapewa nafasi ndogo ya
kutwaa tuzo hiyo.
Angalia rekodi zao za ufungaji kuanzia
November 20,2016 mpaka July 2 2017
0 Comment untuk "Cristiano, Messi na Neymar wapitishwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA (The Best FIFA Men's)"