Leo huko barani Amerika imepigwa michezo kadhaa
ya kufuzu kwa kombe la Dunia.
Brazil ambayo imeshafuzu imeikaribisha timu ya
taifa ya Ecuador na kuiadhibu kwa goli 2 kwa 0.
Goli la kwanza la Brazil limefungwa na Paulinho
baada ya kazi nzuri ya toka kwa kiungo wa Chelsea Willian mnamo dakika ya 69
.
Goli la pili lilifungwa na mchezaji ambae
ameviteka vyombo vya habari akihusishwa kuhamia timu ya Barcelona ya Hispania Philippe
Coutinho dakika ya 76 kufuatia kazi nzuri ya Gabriel Jesus.
Katika mchezo huu Coutinho aliingia dakika ya
58 kuchukua nafasi ya Renato Augusto.
Brazil leo walitumia mtindo wa 4-1-4-1
Matokeo mengine ya CONMEBOL Qualification leo September 1 ni
kama yanavyoonekana:
Venezuela vs Colombia0 - 0
Chile vs Paraguay0 – 3
Magoli: Arturo Vidal (OG) 24’, Victor Caceres 55’ na Richard Ortiz
90’
Uruguay vs Argentina 0 - 0
Peru vs Bolivia2 - 1
0 Comment untuk "Philippe Coutinho na Paulinho waendeleza wimbi la ushindi, brazil 2 Ecuador 0, Chile ya Sanchez yachezea 3 kwa 0"