Mchezaji bora Dunia
raia wa Ureno anaekipiga katika kilabu ya Real Madrid jana aliichukua tuzo ya
mchezaji bora wa kiume wa mwaka wa FiFA mbele ya hasimu wake mkubwa kisoka
Lionel Messi.
Dalili za
Ronaldo kuchukua tuzo hiyo zilionekana wazi Kutokana na mafanikio aliyoyapata
kwa msimu ulioisha wa Laliga,Uefa Champion’s League na Uefa Super Cup.
Ronaldo ndie
mfungaji bora wa ligi ya mabingwa Ulaya kwa msimu ulioisha akimzidi Messi kwa
goli 1.
Ronaldo ametwaa
Laliga msimu ulioisha, pia ametwaa ligi ya mabingwa na pia akiwa Real Madrid
ametwaa Uefa Super Cup.
Hii ni mara ya
pili mfululizo kwa Ronaldo kunyakua tuzo hiyo tangu imeanzishwa mwaka jana .
Pia ameisaidia
timu yake ya Ureno kufanya vizuri kwenye michuano ya kombe la mabara na kufuzu
kwa kombe la Dunia.
Kwa mafanikio hayo
Ronaldo alistahili kutwaa tuzo hiyo.
0 Comment untuk "It’s Cristiano Ronaldo Again the Best FIFA Men’s Player Awards 2017"