Shirikisho la mpira wa miguu nchini
Tanzania TFF limetangaza viingilio katika mchezo ujao wa watani wa jadi Simba
na Yanga siku ya jumamosi October 28.
Viingilio vitakuwa kama ifuatavyo:
Mzunguko: tshs 10000
Jukwaa kuu: tshs 20000
Mchezo huo ambao utapigwa kwenye dimba
la Uhuru jijini Dar es Salaam unasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka ndani
na nje ya Tanzania.
Tambo zimezidi kuongezeka hasa
ukiangalia Matokeo ya michezo ya mwisho ya timu hizo ambapo Simba waliitandika
Njombe mji goli 4 – 0 huku Yanga nao wakiitandika Stand United ya Shinyanga kwa
goli 4 – 0.
Tukurudi kwenye ‘performance’ ni
kama timu zote ziko sawa kwa maana zote zimecheza michezo 7 na kushinda
kushinda 4, kutoka sare 3 na zote zina pointi 15.
Simba yenyewe inaonekana kuwa na
safu kali zaidi ya ushambuliaji kwa mujibu wa takwimu ambazo zipo katika
michezo hiyo saba Simba imefunga magoli 19 wakati yanga ikiwa imefunga magoli
10 pekee.
Kwa upande wa ulinzi Yanga wao wapo
vizuri zaidi ya Simba kwa kuruhusu magoli matatu tu katika michezo saba wakati
Simba wao wameruhusu magoli 4.
Tutegemee mchezo ambao utakuwa na
ushindani wa hali ya juu, ukiingalia Simba imeleta kocha msaidizi ambae wadau
wanategemea atakuja na mbinu za ziada zitakazoweza kuimaliza Yanga.
Huku
Yanga nao wakiwa wamezinduka kutoka kupata ushindi wa kubahatisha mpaka ushindi
wa uhakika.
0 Comment untuk "Kuziona Simba na Yanga jumamosi Tshs.10000 uwanja wa Uhuru"