Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF), limemtua Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika – CHAN.
Rais Karia ameteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe 26 wanaounda kamati hiyo yenye jukumu la kuhakikisha maandalizi ya mashindano hayo yanakwenda vizuri.
Wakati huohuo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodegar Tenga ameteuliwa kushika nafasi ya Makamu wa Rais kwenye kamati ya maendeleo ya soka la ufukweni na Futsal.
Sambamba na uteuzi huo, Tenga pia ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Maendeleo na Ufundi ya CAF yenye wajumbe 17.
Naye Lina Kessy kutoka Tanzania ameteuliwa katika kamati ya watu 15 ya maandalizi ya soka la wanawake wakati Mtanzania mwingine Paul Gaspar Marealle akiteuliwa kwenye kamati ya tiba.
0 Comment untuk "Watanzania waula uteuzi Caf, yupo Karia, Tenga Lina Kessy pamoja na Paul Gaspar Marealle"