Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini
England timu ya Chelsea jana walifanya kile Washabiki wake wanahitaji baada ya
kuwapooza machungu ya UEFA Champions League ya kufungwa 3 – 0 na SSC Napol ya
Italia.
Chelsea jana walifanikiwa kuvuna
pointi 3 muhimu na kuikaribia kwa karibu timu ya man Utd katika nafasi ya 2
baada ya kuchapa goli 1 kwa 0 na kufikisha pointi 22 nyuma ya Utd na Tottenham zenye
pointi 23.
Goli la Chelsea lilifungwa kwa
kichwa na Morata katika dakika ya 55 baada ya krosi safi toka upande wa kulia
wa Chelsea ikichongwa na Cesar Azpilicueta.
Kitu kizuri kwa upande wa Chelsea ni
kushusha kwa presha ya kutaka kumfukuza Conte, pia na kufanikiwa kumziba mdomo
kocha mwenye maneno mengi sana wa Man Utd.
matokeo mengine:
Millionaire Ads
matokeo mengine:
Tottenham Hotspur 1 - 0 Crystal
Palace
Manchester City 3 - 1 Arsenal
Everton 3 - 2 Watford
0 Comment untuk "Conte Amfunga mdomo Jose Mourinho, Chelsea sasa waipumulia UTD kwa karibu"