Manchester City msimu huu ni wa moto
na kila timu inayokutana nayo ni kipigo tu.
Hayo yamejidhihirisha katika michezo
11 ya ligi kuu nchini England baada ya kushinda michezo 10 na kutoka sare
mchezo mmoja dhidi ya Everton.
Mchezo wa jana ulianza kwa kasi
lakini man C walicheza kwa mipango zaidi na dakika ya 19 Fernandinho alimpasia Kevin
de Bruyne na kuwapunguza mabeki watatu wa Arsenal na kumchungulia Petr Cech kisha
kupiga shuti upande wa kushoto wa kipa huyo na kuandika goli la kwanza.
Mpaka mapumziko Man C 1 – 0 Arsenal.
Sergio Aguero alifunga goli la pili
kwa njia ya penati dakika ya 50.
Arsenal kupitia kwa Alexandre
Lacazette dakika ya 65 walipata goli la kufutia machozi baada ya kazi nzuri ya Aaron
Ramsey.
Dakika ya 74 Gabriel Jesus alimalizia
kazi ya David Silva na kuhitimisha ushindi huo mnono ambao ni mwendelezo wa Matokeo
kwa timu ya Man City.
Kwa Matokeo
ya jana City imefikisha pointi 31 na kuziacha Man U na Tottenham zikiwa na pointi 23 kila moja huku Chelsea wakiwa nafasi 4 kwa pointi 22.
0 Comment untuk "Manchester City wawasha indiketa ya ubingwa yaipiga Arsenal 3 na kutengeneza gepu la pointi 8"