Timu ya Tottenham ya Uingereza usiku
wa kuamkia leo imeudhihirishia ulimwengu kuwa ni timu bora kwa sasa ulimwenguni
baada ya kuwafunga mabingwa wa UEFA na Super Cup timu ya Real Madrid ya
Hispania kwa goli 3 – 1.
Delle Alli ndiealiekuwa mwiba
mchungu kwa safu ya ulinzi baada ya kutikisa nyavu mara 2 katika dakika ya 27
akimalizia kazi ya Kieran Trippier na dakika ya 56 alifunga tena baada ya kazi
nzuri ya Eric Dier na kufanya Matokeo kusoma 2 – 0.
Harry Kane alifanya kazi nzur na
kumtengenezea Christian Eriksen ambae
aliifungia timu hiyo goli la 3 daika ya 65.
Dakika ya 80 Ronaldo aliifungia timu
yake goli la kufutia machozi baada ya kumalizia kazi ya Borja Mayoral.
Mchezo mwingine wa kundi H Matokeo yalikuwa
hivi:
Borussia Dortmund 1 - 1 APOEL
Nicosia
Tottenham sasa 95% imefuzu kwa 16
bora kwani timu 2 za chini zina pointi 2 kila moja na zimefungwa goli nyingi
wakati Tottenham yenyewe tayari ina pointi 10 na utofauti wa magoli 7.
Real Madrid wao itabidi wasubiri
mchezo mmoja washinde ndio wajihakikishe kutinga 16 bora fainali.
Kwa sasa real Madrid wana pointi 7.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Dele Alli aoongoza mauaji, Tottenham ikiiua Real Madrid goli 3 na kukata tiketi ya 16 bora"