Soma taarifa iliyotolewa leo kwa
vyombo vya habari na bosi wa kitengo cha habari ndani ya Simba.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Benchi la ufundi la klabu ya
Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya marekebisho kwenye eneo la
unahodha wa timu.
Katika marekebisho hayo yaliyoridhiwa
na uongozi wa klabu,beki wa kimataifa Mzimbabwe Method Mwanjale ameteuliwa kuwa
nahodha mpya wa timu ya Simba,akichukua nafasi ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa
mchezaji mwandamizi kwenye kikosi hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika
kusini kujiandaa na msimu mpya unaotarajiwa kuanza
mwezi ujao.
Kwenye mabadiliko hayo ya
kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania
na klabu ya Simba kwa msimu huu,Mohammed Hussein(Tshabalala)na John Raphael
Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu hiyo.
Klabu inamshukuru sana Nahodha
wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi
nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa Timu.
Kwa sasa kikosi chetu kinaendelea
na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko kambini Eden Vale Johannesburg
nchini Afrika kusini.
IMETOLEWA NA..
*HAJI S MANARA*
MKUU WA HABARI WA SIMBA SC
*SIMBA NGUVU MOJA*
0 Comment untuk "Mwanjale apewa unahodha Simba, Bocco nae apewa cheo, Mkude apongezwa"