Mshambuliaji
wa Barcelona Neymar, 25, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na
Paris Saint-Germain na huenda akakamilisha uhamisho wa pauni milioni 197 wiki
ijayo. (RMC)
PSG
watawapa Barcelona Angel Di Maria, 29, kama sehemu ya mkataba wa kumsajili
Neymar, ili kupunguza kodi ya kutengua kifungu cha uhamisho cha mchezaji huyo
wa Brazil. (AS)
Iwapo
Neymar ataondoka, Barcelona wataamua kuwawinda wachezaji watatu kutoka EPL- Philippe
Coutinho, 25, wa Liverpool, Eden Hazard, 26, wa Chelsea, na Delle Alli, 21 wa
Tottenham kuziba pengo. (Mirror)
Barcelona
wana wasiwasi kuwa bei kubwa ya kumsajili Philippe Coitinho kutoka Liverpool
huenda ikawakatisha tamaa. (AS)
Kiungo
wa Barcelona Andres Inisesta, 33, amesema ni Neymar pekee anayeweza kuzungumzia
kuhusu hatma yake, akisema hadhani kama euro milioni 200-300 hazina manufaa
yoyote kwa klabu bila Neymar mwenyewe. (Marca)
Monaco
wanasisitiza kuwa hawatamuuza Thomas Lemar, 21, licha ya Arsenal kupanda dau la
tatu la takriban pauni milioni 45 kumtaka kiungo huyo. (Telegraph)
Manchester
City watampa Alexis Sanchez, 28, mshahara wa pauni 320,000 kwa wiki akijiunga
nao kutoka Arsenal. (Mail)
Kipa
wa Manchester City Claudio Bravo amesema Alexis Sanchez atapokelewa kwa mikono
miwili akiamua kwenda Etihad. Bravo na Sanchez wote wanachezea timu ya taifa ya
Chile. (24 Horas)
Southampton
wamedhamiria kutomuuza beki wao Virgil van Dijk, 26, na watamrejesha katika
kikosi cha kwanza licha ya kuachwa katika kikosi kilichokwenda mazoezini
Ufaransa wiki hii (Telegraph)
West
Ham watakataa dau lolote la kumtaka kiungo mshambuliaji wake Manuel Lanzini,
24. (Evening Standard)
Swansea
wanakabiliwa na ushindani kutoka Leeds United katika kumsajili Alvaro Negredo,
31, aliyecheza kwa mkopo Middlesbrough msimu uliopita. (Mirror)
Manchester
United wamenza mazungumzo ya mkataba mpya na Ander Herera, 27, ili kuzuia
Barcelona kumnyatia kiungo huyo. (Express)
Manchester
United wamerejea tena katika kumfuatilia winga wa Inter Milan Ivan Perisic, 28,
lakini wana wasiwasi huenda wakamkosa kwa kuwa wamepoteza muda mwingi
kumfuatilia Gareth Bale, 28, wa Real Madrid. (Independent)
Meneja
wa Inter Milan Luciano Spalletti anadhani mkataba wa Ivan Perisic kwenda Old
Trafford haupo tena kutokana na kusuasua kwa mazungumzo kati ya Man Utd na
Inter hivi karibuni. (Premium Sport)
Gareth
Bale atakataa hatua ya Real Madrid kumuuza kwenda Manchester United kwa sababu
hana mpango wa kuondoka Madrid. (Times)
Mchezaji
kinda kutoka Brazil, Gabriel Martinelli, 16, anafanya majaribio na Manchester
United akitarajia kukamilisha uhamisho wake kutoka Ituano. (Manchester Evening
News)
Liverpool
wameacha kumfuatilia kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, na huenda wakarejea
tena msimu ujao ambapo inaaminika huenda wakaweza kumsajili kwa pauni milioni
48. (Liverpool Echo)
Liverpool,
Arsenal na Tottenham, zote zinamnyatia kiungo wa Barcelona Rafinha msimu huu.
(Mundo Deportivo)
Arsenal
wanataka kumsajili kiungo Jakub Jankto, 21, kutoka Udinese. (SportItalia)
Chelsea
watalazimika kutoa takriban pauni milioni 17.9 kama wanataka kumsajili kiungo
wa Inter Milan Antonio Candreva. (Daily Star)
Everton
watataka kumsajili kiungo wa Nice, Jean Seri, 26, ambaye pia ananyatiwa na
Arsenal, ikiwa watashindwa kumpata Gylfi Sigurdsson, 27, kutoka Swansea.
(L’Equipe)
Nb:
tetesi hizi ni Cop $ Paste kutoka https://web.facebook.com/SalimKikeke/posts/1011327079004754
Millionaire Ads
0 Comment untuk " TETESI ZA SOKA ULAYA JUMAMOSI 29.07.2017"