Millionaire  Ads

AVEVA KABURU MAMBO MAGUMU, WARUDISHWA TENA RUMANDE HADI SEPT 8


RAIS WA TIMU YA Simba na makamu wake leo wameshindwa tena kwemye kesi yao na kurudishwa rumande hadi September 8.

Hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu Victoria Nongwa  amesema leo mahakamani hapo kwamba ameiahirisha kesi hiyo ili kupisha uchunguzi wa nyaraka zilizokusanywa.
Hakimu huyo amewataka mawakili wa upande wa Serikali kufanye haraka  kufuatilia nyaraka zilizokusanywa, ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashitaka matano yakiwemo ya utakatishaji fedha, ambayo hayana dhamana na wote wapo rumande gereza la Keko tangu Juni 29.
Wawili hao leo waliletwa tena Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar es Salaam kwa mara ya saba tangu Takukuru ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) iwatie hatiani na kusomewa tena mashitaka hayo kabla ya Hakimu Victoria Nongwa kuiahirisha tena kesi hiyo hadi Agosti 16, mwaka huu.
Millionaire  Ads

Share :

Facebook Twitter Google+ Lintasme

Related Post:

0 Comment untuk "AVEVA KABURU MAMBO MAGUMU, WARUDISHWA TENA RUMANDE HADI SEPT 8"

Back To Top