Huko Mbeya wakicheza kwa tahadhari kubwa huku wakikumbuka
vipigo viwili mfululizo walivyopata katika mechi zilizopita, timu ya Tanzania
Prisons imeadhibu simba goli 2 – 1 katika mechi ya kukamilisha raundi ya
kwanza.
Mchezo ulianza kwa simba kuliandama lango la wenyeji wao
huku tukimshudia Mavugo, na Mnyate wakipoteza nafasi za wazi ambazo zingeipatia
simba uongozi mapema, iliwachukua simba dakika 43 kujipatia goli kupitia kwa
Mnyate baada ya kuunganisha kwa kichwa pasi safi ya Kichuya.
Kipindi cha pili Tanzania Prisons waligeuza aina ya mchezo
na kuwazua simba kupiga krosi huku wakishambulia kwa kushtukiza na mnamo dakika
ya 47’ na 64’ kupitia kwa Hangayaa .
Hadi mwisho wa mchezo huo Tanzania Prisons 2 simba 1.
Shinyanga mambo yamewaendea vizuri Azam Fc baada ya kupata
ushindi wa kwanza mkubwa katika msimu huu baada ya kuitandika bila huruma timu
ya Mwadui kwa magoli 4 – 1.
Mwadui ndio waliotangulia kuliona lango la Azam dakika ya 30
kupitia kwa Hassan Kabunda, mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Mwadui 1 Azam
0.
Kipindi cha pili 54’ John Bocco aliisawazishia Azam, dakika
ya 71 Shaaban Idd alifunga goli la pili dakika 74 Shaaban Idd alifunga la tatu
na alifunga tena la nne na la tatu kwake.
Millionaire Ads
0 Comment untuk "Azamu yamuenzi Mzee Said Mohamed Abeid kwa ushindi mnono, Simba yashikwa sharubu Mbeya"