Safari
ya baadhi ya viongozi wa Azam kwenda Ghana hatimae imezaa matunda baada ya kuizidi ujanja Hearts of Oak na kumsajili golikipa wa timu ya
taifa ya Ghana kwa wachezaji wa ndani Razak Abalora kutoka WAFA SC.
Kipa huyo namba moja wa timu ya WAFA
tangu 2016 amekuwa na msimu mzuri baada ya kucheza michezo 22 kati ya michezo hiyo michezo 12 amedaka bila kuruhusu
nyavu zake kutikiswa.
Razak alichukua nafasi ya Felix
Annan ambae alitolewa kwa mkopo kwenda timu ya Asante Kotoko.
Razak amecheza jumla ya michezo 22
msimu huu na kufanikiwa kuisaidia timu yake ya WAFA kuwa katika nafasi ya pili.
Razak Abalora amesaini mkataba wa
miaka mitatu ndani ya Azam na huenda akawa ndie mbadala wa Aish Manula.
Razak Abalora anakamilisha idadi ya
makipa 4 ndani Azam mpaka, makipa wengine ni Benedict Haule, Menata Boniphace Pamoja na mkongwe Mwadini Ali
Millionaire Ads
0 Comment untuk " Azam yanasa bonge la kipa kuziba pengo la Manula"